Radio
16:30 - 17:00
Kyra Harris Bolden anakuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwahi kuhudumu mahakama kuu jimbo la Michigan nchini Marekani
Bolden mwenye umri wa miaka 34 atajiunga na mahakama hiyo mwezi Januari baada ya muda wake wa uwakilishi kwenye bunge kumalizika. Anajaza kiti kilichoachwa wazi na Jaji Bridget McCormack. Na kama Bolden anataka kushikilia kiti hicho hadi 2028 lazima agombee katika uchaguzi wa 2024
19:30 - 20:29
Live talk: Wachambuzi watoa mtazamo wao kuhusu timu za Afrika ya michuano ya duru ya pili kwenye kombe la dunia huko Qatar
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
21:00 - 21:30
Mjadala mkubwa waendelea Kenya kuhusiana na kuagizwa kwa vyakula vya GMO nchini, ili kukabiliana na uhaba wa chakula uliyopo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.