Radio
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump atangaza kugombania urais uchaguzi wa 2024
Wakati kura zikiwa hazijamalizika kuhesabiwa za uchaguzi wa bunge wa katikati ya muhula wa Marekani wa 2022, rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump ametangaza nia ya kugombea urais kwa mara nyingine kupitia chama cha Republikan katika uchaguzi wa 2024.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais 2024 kupitia chama cha Republican
Jitihada mpya za Trump zinaanza takriban miaka miwili baada ya kuwahimiza wafuasi wake kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 ambao ulisababisha ghasia mbaya katika majengo ya bunge la Marekani hapo Januari 6, 2021
Katibu Mkuu wa NATO anasema mlipuko karibu na mpaka wa Ukraine huenda ulisababishwa na kombora la Ukraine lililofyatuliwa dhidi ya Russia
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels baada ya mkutano wa Baraza la Atlantiki Kaskazini, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg anasema washirika wote wa NATO walikubaliana na tathmini hiyo ambayo ilitokana na uchunguzi wa awali na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea.