Radio
Kenyatta aeleza masikitiko kuona maelfu ya watu waliofurushwa makwao DRC
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta Jumatano alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kwa haraka, na kutanzua mzozo unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako mapigano kati ya jeshi na waasi wa M23 yamepamba moto tena.
Suala la mahari lajadiliwa katika bunge la Rwanda
VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo.
Jioni: Rais wa Kenya Dkt. William Ruto anataka wabunge wa chama chake kutofikiria kuondoa kikomo kwa mhula wa rais
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Visa vya Ebola vyaendelea kuripotiwa kwenye wilaya kadhaa za Uganda, huku maafisa wa afya wakilalamikia mazingira duni ya kazi.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.