Radio
06:00 - 06:29
Mataifa mengi maskini yanapata shida kutafuta fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa-UNDP
Mkuu wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa aonya kwamba mataifa mengi maskini yanapata shida kutafuta fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu ya mzigo mkubwa wa madeni waliyonayo.
19:30 - 19:59
Jioni: Kura zinaendelea kuhesabiwa katika uchaguzi wa katikati ya mhula Marekani, hakuna chama kina uhakika wa kudhibithi bunge kufikia sasa
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
21:00 - 21:29
Yaliyomo kwenye mkataba wa reli ya SGR kati ya Kenya na China yaibua utata
Mkataba wa reli ya standard gauge (SGR) uliotiwa saini na Kenya unawapa mamlaka makubwa wakopeshaji wake wa Uchina, ikiwa ni pamoja na kutaka usuluhishi wa mzozo wowote utakaofanyika Beijing, stakabadhi zilizotolewa na serikali baada ya miaka ya usiri zimeonyesha.