Upigaji kura wa mapema unaendelea katika majimbo kadhaa, Makamu Rais na mgombea urais Kamala Harris akizungumza na waandishi wa habari amezidisha ukosoaji kwa mpinzani wake wa kisiasa Rais wa zamani Donald Trump.
Uchaguzi wa rais wa Novemba 05 unasababisha wasiwasi kwa karibu robo tatu ya wale waliohojiwa na chama cha wanasaikolojia cha Marekani.
Baadhi ya Wamarekani tayari wamefanya maamuzi kuhusu rais wanayemtaka huku upigaji kura wa mapema ukiwa unaendelea katika majimbo mengi.
Majimbo hayo ambayo ni maarufu kama ‘Swing States’ ni muhimu kushinda kuingia White House mwaka 2024.
Idadi ya wapiga kura wanawake imekuwa ni juu zaidi kuliko kwa wanaume katika uchaguzi wa rais Marekani tangu mwaka 1984. Kwa mujibu wa Center for Women in American Politics, wanawake wamekipigia kura chama cha Democratic dhidi ya Republican katika kila uchaguzi wa rais tangu mwaka 1992.
Fursa mbalimbali zilizowasilishwa na vyama vikuu viwili – Demokratic na Republican – vina uhakika kuwa rais ajaye atakuwa anatokana na chama kimoja wapo kati ya hivyo, kama ilivyokuwa kwa marais wote tangu 1856. Utawala wa mfumo wa vyama viwili unaweza kuonekana ni kitu cha ajabu.
Kabla ya Kamala Harris kuingia katika kinyang’anyiro cha urais ukusanyaji maoni umeonyesha kuwa karibu nusu ya wapiga kura hawakuwa wanafurahishwa na wote Rais Biden na Rais wa zamani Trump.
Wamarekani wako tayari kupiga kura mwezi Novemba katika uchaguzi ambao unatarajiwa kuwa na ushindani wa karibu sana katika nafasi ya urais. Jeff Swicord amezungumza na mfuasi wa Trump na Harris ili kupata mawazo yao na uzeofu wao. Hubbah Abdi anaisoma ripoti kamili.
Seneta wa Marekani JD Vance, mgombea mwenza wa Donald Trump wa chama cha Republikan, alishindana na Gavana wa Minnesota Tim Walz, ambaye ndiye mgombea mwenza wa Kamala Harris wa chama cha Demokratik katika mdahalo wa televisheni ya kitaifa siku ya Jumanne.
Kinyume na ilivyo katika nchi nyingine, Marekani haina sheria ya ukomo wa muda maalum wa kampeni za urais.
Januari 15, msimu wa uchaguzi wa rais Marekani 2024 utazinduliwa rasmi kwa mikutano ya vyama ya kuchagua wagombea huko Iowa.
Jibu hapana mpaka pale wanapokuwa maraia. Kupata uraia ni mchakato mrefu ambao unaanza na kupata “green card” ambayo pia inajulikana kama kadi ya ukaazi halali wa kudumu. Sunday Shomari wa VOA anaeleza mchakato huo…
Hapana. Kazi iko wazi kwa wale wana sifa zilizotajwa katika Katiba ya Marekani.
Ufyatuaji risasi katika shule ya sekondari jimboni Georgia siku ya Jumatano ilikuwa ni ukumbusho mkubwa kwamba silaha zinawaua Wamarekani zaidi kuliko katika nchi yoyote kubwa yenye kipato cha juu, kwa mujibu wa watalaamu wa afya.
Baadhi ya familia za Gold Star zimeelezea uungaji mkono wao Jumapili kwa rais wa zamani Donald Trump, baada ya kukosolewa kwa kupiga picha na video katika sehemu iliyowekewa kizuizi kwenye Makaburi ya Kitaifa ya Arlington wiki iliyopita.
Kamala Harris ameahidi kuchukua msimamo mkali juu ya uhamiaji katika eneo la mpaka wa kusini wa Marekani na kusema hatozuia upelekaji silaha kwa Israel.
Sheria ya Huduma Nafuu ya Afya ACA ambayo pia inajulikana kama “Obamacare,” imeongeza fursa ya huduma za afya kwa mamilioni ya Wamarekani, lakini haiko bayana nini mustakabali wa program chini ya rais ajaye.
“Alikuwa ni malkia wa mpakani. Mara ghafla anasema yeye siyo tena malkia wa mpakani,” alisema Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Mwezi mmoja tu baada ya Rais Joe Biden kutangaza hatawania tena kuchaguliwa kwa muhula mwingine, Kamala Harris alikubali uteuzi wa chama cha Democratik kuwa mgombea urais.