Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 10:59

Uchaguzi Mkuu wa Rais Marekani: Tofauti kati ya kura za wajumbe na kura ya umma


Wananchi wajitokeza kupiga kura nchini Marekani.
Wananchi wajitokeza kupiga kura nchini Marekani.

Wamarekani wanakwenda kwenye vituo hivi leo Novemba 5 kupiga kura kumchagua rais ajaye wa Marekani. Hata hivyo, hesabu ya kura kitaifa haiamui mgombea gani anashinda kuingia White House. Electoral College yaani kura za wajumbe ndiyo zenye kauli ya mwisho...

Hata hivyo, hesabu ya kura kitaifa haiamui mgombea gani anashinda kuingia White House. Electoral College yaani kura za wajumbe ndiyo zenye kauli ya mwisho. Lakini utaratibu huu unafanya kazi vipi.

Wakati wagombea wanaposhinda kura ya umma, ina maana wamepata kura nyingi zaidi kuliko mshindani wake.

Lakini hivi sivyo rais wa Marekani anavyochaguliwa. Wakati Waanzilishi wa taifa hili la Marekani walipoanzisha mchakato wa kura za wajumbe mwaka 1787, walitaka kuweka uwiano wa madaraka kati ya majimbo na kuzuia wagombea ambao hawastahili kushika madaraka ya uongozi.

Electoral College iliundwa kuleta maafikiano, na kuwa kama kizuizi kati ya uchaguzi na uteuzi wa rais.

Electoral College hivi sasa ina wajumbe 538, na wajumbe hao wamegawanyika katika majimbo yo te 50 ya Marekani kulingana na ukubwa wa wajumbe katika bunge, ambapo nayo wingi wa idadi ya watu. California, kwa mfano, ina wajumbe 54, wakati jimbo la Wyoming ambalo lina watu wachache lina wajumbe watatu tu.

Ili kuwa rais, mgombea anahitaji kupata walau kura 270 za wajumbe kati ya 538.

Majimbo 48 na District of Columbia jiji kuu la Marekani wana mfumo ambao mshindi anachukua kura zote za wajumbe, kwahiyo mgombea urais mwenye kura nyingi katika jimbo husika anachukua kura zote za wajumbe.

Majimbo mawili – Maine na Nebraska – wanatenga kura za wajumbe kwa mgombea mwenye kura nyingi zaidi katika kila wilaya ya uchaguzi, kwahiyo matokeo yanaweza kuwa ni kugawana kura.

Inapokuja kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Marekani, kura za umma kote nchini hazijalishi. Kuna uwezekano wa kuwa na rais ambaye ana kura chache za umma kuliko mgombea mwingine.

Hili limetokea mara tano katika historia. Donald Trump alikuwa rais mwaka 2016 licha ya kupata kura chache milioni 2.;9 kuliko kura za Hillary Clinton. George W. Bush alishinda kuingia White House mwaka 2000 licha ya kuwa na kura chache kwa 540,000 kuliko Al Gore.

Mchakato “usio wa moja kwa moja wa uchaguzi” nchini marekani unaendelea kukabiliwa na uchunguzi. Kumekuwepo na zaidi ya mapendekezo 700 kuufuta au kuufanyia mageuzi mfumo wa Electoral College, lakini hata moja uliofanikiwa.

Kwa hakika tutafahamu rais ajaye wa nchi muda mfupi baada ya siku ya uchaguzi, lakini wajumbe kutoka kila jimbo hawatapiga kura rasmi mpaka mwezi Desemba.

Ingawaje mchakato wa Electoral College umeandikwa katika Katiba, hausemi katika katiba lazima wapige kura kulinngana na jinsi wapiga kura wa jimbo walivyopiga kura. Mamlaka hayo yanaacwa kwa majimbo.

Mpaka hivi sasa, wajumbe 90 wasio na imani wamempigia kura mgombea urais tofauti, ingawaje ni mmoja tu amewahi kumpigia kura mgombea wa chama ambacho kimeshindwa katika uchaguzi wa karibu. Hili halijawahi kujitokeza katika uchaguzi, lakini linabainisha hali ya kutotabirika kwa mifumo ya uchaguzi ya Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG