Chama cha Republican kilishinda viti vingi katika bunge la seneti kwa kupata viti 51 kati ya 100 katika uchaguzi wa Jumanne. Udhibiti wa Baraza la Wawakilishi ambalo kwa sasa linashikiliwa na Warepublican ulikuwa bado haujaamuliwa kufikia mapema Jumatano.
Viti vyote 435 katika Baraza la Wawakilishi vilikuwa kwenye kinyang’anyiro katika uchaguzi nchini Marekani kwa vipindi vipya vya miaka miwili, wakati viti 34 kati ya 100 katika Seneti viligombewa kwa muhula mpya wa miaka sita.
Kabla ya siku ya uchaguzi, Democrats walikuwa na udhibiti mdogo wa Seneti, na Republicans katika Baraza la Wawakilishi. Ushindi muhimu wa Republican kwa viti vya Seneti katika majimbo ya West Virginia na Ohio unawaweka katika nafasi ya kurudi kushikilia wingi wa viti bungeni.
Katika Baraza la Wawakilishi, Republicans walishikilia viti 220 kwa 212, na viti vitatu vilivyo wazi vinaingia kwenye uchaguzi. Udhibiti wa bunge bado hauja-thibitishwa. Udhibiti wa bunge huenda usijulikane kwa siku kadhaa, kwa kuwa jimbo la California mara nyingi linachukua siku kadhaa kuhesabu kura, na kurudia kuhesabu pamoja na uchaguzi wa marudio kwa wagombea wanaofungana inaweza kuchukua wiki kadhaa kutatua.
Uchunguzi wa kisiasa wakati wote wa kampeni za uchaguzi umeonyesha wapiga kura, walio wengi kama vile katika kinyang’anyiro cha kuingia White House, kati ya Kamala Harris na Donald Trump wamegawanyika katika upendeleo wao wa kisiasa kwa udhibiti wa bunge.
Katika kura za maoni zilizofanywa na Reuters ba Ipsos mwezi Oktoba ziligundua asilimia 43 ya wapiga kura waliosajiliwa watamuunga mkono mgombea wa Republican katika maeneo yao, wakati asilimia 43 wangemuunga mkono mgombea wa Democratic.
Forum