Biden alimkaribisha Trump kwa ziara ya kawaida, kuonyesha kuwa Januari 20 kutakuwa na makabidhiano ya amani ya madaraka katika demokrasia ya marekani kati ya kiongozi wa sasa wa Marekani na mtendaji mkuu anayeingia katika wadhifa huo.
Utamaduni wa kumkaribisha rais anayeingia madarakani ni moja ya jambo ambalo Trump hakulifanya baada ya Biden kumshinda mwaka 2020. Mkutano wa Jumatano kati ya watu hao wawili ulikuja wakati Trump akichukua hatua kuunda utawala wake.
“Ndiyo, Bwana Rais-mteule na rais wa zamani Donald Trump, hongera sana na natazamia kama nilivyosema, kuwa na makabidhiano ya amani ya utawala. Tutafanya kila kitu tunachoweza kukidhi kile unachokihitaji na ndiyo tutapata fursa ya kuzungumza kuhusu baadhi ya mambo hayo hivi leo. Karibu, karibu tena.”
“Ahsante sana. Siasa ni ngumu. Na katika nyakati nyingi, si sehemu nzuri sana katika dunia. Lakini ni dunia nzuri ya leo na nashukuru sana. Kipindi cha mpito kitakuwa hakina tatizo mambo yatakwenda vizuri na nashukuru sana kwa hilo, Joe,” amesema Rais-mteule Trump.
Mke wa Rais Jill Biden alijiunga na mume wake kumlaki rais-mteule alipowasili White House. White House imesema alimpa Trump barua ya pongezi aliyomuandikia mke wake, Melania, na kuelezea kuwa timu yake iko tayari kusaidia katika kipindi cha mpito.
Forum