Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:41

Kwa nini uchaguzi wa rais Marekani hufanyika siku ya Jumanne?


Makamu Rais na mgombea urais wa Demokratiki Kamala Harris (Kushoto) na Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa Republikan.
Makamu Rais na mgombea urais wa Demokratiki Kamala Harris (Kushoto) na Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa Republikan.

Je umewahi kufikiria kwanini uchaguzi wa rais wa Marekani mara zote hufanyika wakati wa majira ya kipupwe na siku ya Jumanne? 

Baraza la Wawakilishi la Marekani
Baraza la Wawakilishi la Marekani

Hii kitadamuni inarejea nyuma takriban miaka 200 iliyopita wakati Marekani ilipokuwa ikionekana tofauti sana na ilivyo hivi leo. Kennes Bwire anatupasha zaidi.

Mwishoni mwa miaka ya 1700 na mwanzoni mwa 1800, majimbo ya Marekani yaliitisha uchaguzi wa rais katika kipindi cha siku 34, ambayo uligeuka kuwa na matatizo.

Watunga sera haraka waligundua kwamba majimbo ambayo yalifanya uchaguzi wa mapema katika kipindi hicho cha siku 34 huenda yaliingilia ukusanyaji maoni wa umma na kushawishi matokeo ya kura katika majimbo ambayo yalifanya uchaguzi wao baadaye.

Suluhisho lilikuwa kuunganisha mchakato wa uchaguzi kwa kuchagua siku maalum ambapo kila mtu atapiga kura.

Mwaka 1845, Bunge lilipitisha sheria iliyoamua siku ya Jumanne baada ya Jumatatu ya kwanza ya mwezi Novemba kuwa ni siku ya uchaguzi – tarehe ambayo imebaki hadi hivi leo.

Lakini nini hasa lilifikisha Bunge katika hatua hii?

Sehemu kubwa ya Marekani ilikuwa ya mashambani katika karne ya 19, na maisha yalizunguka katika taratibu za kawaida ya upandaji, mavuno na kuuza mazao.

Jumatano, ambayo ndiyo inaonekana kama ndiyo siku ya soko kwa wakulima, haraka siku hiyo haikuangaziwa. Jumapili ilitengwa kwa watu kwenda kanisani, kwahiyo siku hiyo pia haikuwa njia nzuri mbadala.

Kwasababu watu wengi waliishi mbali na vituo vya kupigia kura, Bunge pia lilitaka kuwapa wapiga kura muda wa kusafiri kwenda kwenye vituo.

Jumanne ikawa ndiyo siku muafaka, na iliruhusu muda wa kutosha kusafiri baada ya kwenda kanisani bila ya kuathiri shughuli zao kuu za kila siku.

Wakulima pia walikuwa na ushawishi kuhusu siku ya uchaguzi katika mwezi, kama ni majira ya machipuko au ya joto ambayo kitamaduni ilikuwa ni msimu wa upandaji, wakati mwishoni mwa majira ya joto na mwanzoni mwa majira ya kipupwe ilikuwa ni kipindi cha mavuno.

Kwahiyo, ilieleweka vyema kuitisha uchaguzi mwezi Novemba, wakati mavuno yalikuwa kwa kawaida yamekwisha fanyika, lakini ni wakati wa hali ya hewa ya baridi kali ndiyo inaanza kuingia.

Siku hizi, nchi nyingi kote duniani huitisha chaguzi zao siku ya Jumapili, lakini Marekani bado imeendelea na mpango wake wa kitamaduni wa siku ya uchaguzi kuwa Jumanne.

Baadhi wamesema imekuwa ni rahisi kwa nguvu kazi ya sasa ya Marekani, ambapo kwa kawaida Jumatatu mpaka Ijumaa ni siku za kazi, kupiga kura, ikiwa ni pamoja na Siku ya Uchaguzi iwe ni sikukuu ya serikali kuu.

Forum

XS
SM
MD
LG