Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 19:22

Harris na Trump wapeleka kampeni zao kwenye majimbo yasiotabirika


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa kwenye kampeni mjini Greensboro, North Carolina.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa kwenye kampeni mjini Greensboro, North Carolina.

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris, na rais wa zamani Donald Trump Jumatano wamepeleka kampeni zao kwenye majimbo yenye ushindani mkubwa, ikiwa juhudi ya kushawishi wapiga kura zikiwa zimebaki siku 6 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ambao umekuwa vigumu kutabiri.

Harris, mgombea wa Democratik, na Trump, ambaye ni mgombea wa Repablikan, wote wawili walielekea kwenye jimbo la North Carolina kabla ya kuelekea Wisconsin, wakati Harris pia akifanya kampeni kwenye jimbo jingine muhimu mashariki mwa Marekani la Pennsylvania.

Majimbo hayo matatu ni muhimu yakiwemo pia Michigan, Georgia, Nevada na Arizona, ambayo wagombea wote wawili wanaamini ni muhimu katika kuamua mshindi wa urais kwenye uchaguzi wa Jumanne. Kura ya maoni kuhusu majimbo hayo 7 pamoja na kitaifa zinaonyesha ushindani wa karibu kati ya Harris na Trump.

Kufikia sasa karibu watu milioni 57 wamepiga kura hapa Marekani, kwenye vituo vya kupigia kura au kwa njia ya posta, huku maelfu wengine wakiendelea kupiga kura za mapema, japo kuna baadhi ambao bado hawajafanya maamuzi yao.

Forum

XS
SM
MD
LG