Mdahalo huo uliowakutanisha ana kwa ana kwa mara ya kwanza, kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Novemba.
Jukwaa liliandaliwa kwa kile ambacho huenda ikawa ni muda muhimu wa kampeni kuelekea uchaguzi wa rais wa Marekani Novemba 5.
Wagombea hao wawili hawajawahi kukutana au hata kuzungumza kwa simu, lakini Jumanne walisimama umbali mdogo kati yao nyuma ya kizimba katika National Constitution Center huko Philadelphia.
Malumbano hayo yalidumu kwa dakika 90 na yaliyoendeshwa watangazaji wawili wa kituo cha televisheni cha ABC, David Muir na Linsey Davis.
Mdahalo huu kati ya wagombea wa urais kwa kile kinachoweza kuwa ni mdahalo wa kipekee wa kampeni hii.
Tukio hili limefanyika wiki nane kabla ya siku Rasmi ya Uchaguzi lakini siku chache tu kabla ya upigaji kura wa mapema utaanza katika baadhi ya majimbo 50 ya nchi hii.
Forum