Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 14:22

Marekani yasema vitisho vya bomu wakati wa uchaguzi vilianzia Russia


Kituo cha kupigia kura Marekani.
Kituo cha kupigia kura Marekani.

Vitisho  kadhaa vya mabomu vilivyotumwa kwenye vituo vya kupigia kura kote Marekani vinaonekana vinatoka Russia, kulingana na uangalizi mpya kutoka maafisa wa usalama wa serikali kuu na majimbo.

Vitisho vya awali vilitokea Jumanne na kusababisha kusimamishwa kwa muda upigaji kura kwenye baadhi ya vituo katika sehemu za kusini mashariki mwa jimbo la Georgia. Lakini maafisa kwa haraka walithibitisha havikuwa vya kweli. “tulitambua chanzo chake kuwa Russia,” alisema waziri wa mambo ya nje wa Georgia Brad Raffenspenger, alipoongea na wanahabari.

Idara ya ujasusi ya FBI Jumanne ilisema kuwa ilifahamu kuhusu tishio la mabomu kwenye vituo vya kupigia kura katika majimbo kadhaa, na kuongeza kuwa baada ya kufuatilia taarifa hizo, zilionekana kuanzia Russia. Afisa mmoja wa serikali aliithibitishia VOA kwamba kando na Georgia, vitisho vya mambomu pia vilitumwa kwenye majimbo muhimu ya Michigan na Wisconsin.

Inashukiwa kuwa zilikuwa juhudi za mwisho mwisho za Russia za kuvuruga uchaguzi wa Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG