Radio
16:30 - 17:00
Vijana kutoka Afrika wanatarajia mkutano unaoendelea nchini Marekani utatoa fursa kwa vijana kupata muongozo bora wa mbinu za uongozi
Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris alisema "Ninaamini kwa dhati kwamba ubunifu na ustadi wa viongozi vijana wa Afrika utatusaidia kuunda mustakabali wa dunia. Na kwamba mawazo yao, mawazo yako, ubunifu na mipango yako itanufaisha dunia nzima".
19:30 - 19:59
Raia wawili wa Ethiopia wamewasilisha kesi dhidi ya kampuni mama ya Facebook ya META kuhusu matamshi ya chuki kwenye mitandao ya kijamii
Mtafiti wa zamani wa haki za binadamu wa Amnesty International, Fisseha Tekle ni mmoja wa walalamikaji katika kesi iliyowasilishwa Jumatano na mwingine ni mtoto wa profesa wa chuo kikuu, Meareg Amare ambaye aliuawa wiki kadhaa baada ya machapisho kwenye Facebook kuchochea ghasia dhidi yake