Radio
16:30 - 16:59
Vijana nchini Tanzania wanasema miaka 61 ya Uhuru kwa upande wao kuna changamoto ya ajira hivyo kuzorotesha kasi ya ukuaji wa maendeleo
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ametoa salamu za maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru na amewataka wananchi kutumia siku hii kutafakari pamoja na kuweka dhamira ya kuongeza juhudi za kulipeleka taifa mbele kwa kasi zaidi
19:30 - 20:30
Kombe la dunia: maajabu yatokea tena katika mchezo wa Brazil na Croatia
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
21:00 - 21:29
EU imemuwekea vikwazo mfanyabiashara wa dhahabu wa Ubelgiji, wakuu wa waasi na jeshi la Congo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu DRC
Watu hao 17 yakiwemo makundi ya ADF, CODECO, Mai Mai Yakatumba, M23, FDLR sasa wanakabiliwa na hatua za kuzuiwa EU hadi Disemba 2023 inajumuisha marufuku ya kusafiri na kuzuia mali Baraza la Umoja wa Ulaya (EU) limesema katika taarifa kwa vyombo vya habari