Wafanyakazi wawili wa shirika la misaada lenye makao yake Uingereza la Tearfund waliuawa katika shambulizi dhidi ya msafara wao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, shirika hilo la hisani lilisema Jumatatu.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Libya mjini Tripoli amesema kuwa mpaka muhimu na Tunisia wa Ras Ijdir umefunguliwa Jumatatu, miezi mitatu baada ya kufungwa kutokana na mapambano ya silaha.
Wagombea urais wa Marekani Joe Biden na Donald Trump walikuwa na mdahalo wa CNN wa wagombea urais wa kwanza katika mzunguko huu wa uchaguzi jana Alhamisi.
Shirika la kimataifa la fedha (IMF) Jumatano limesema bodi yake ya utendaji imekamilisha tathmini ya tatu ya mpango wa kuirahisishia Zambia kuendelea kupata mikopo na imeidhinisha mkopo wa mara moja wa dola milioni 569.6.
Shirika la kimataifa la fedha (IMF) Alhamisi limesema bodi yake ya utendaji imeidhinisha ufadhili wa dola milioni 786.2 kwa Tanzania kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mkataba mpya wa kujihami kati ya Russia na Korea Kaskazini unadhihirisha kuimarika kwa mshikamano kati ya mataifa ya kimabavu na inasisitiza umuhimu wa mataifa ya kidemokrasia kuonyesha umoja katika vita dhidi ya udikteta, katibu mkuu wa NATO alisema Jumatano.
Rais wa Russia Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamekubaliana kuimarisha uhusiano kati ya mataifa yao, wakati wa mkutano wao katika siku ya kwanza ya ziara ya Putin mjini Pyongyang Jumatano, vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimesema.
Mashambulizi ya anga ya Israeli Jumanne yameuwa Wapalestina wasiopungua 17 katika kambi mbili za wakimbizi za kihistoria huko Ukanda wa Gaza na vifaru vya Israeli viliingia ndani zaidi katika mji wa kusini wa Rafah, wakazi na wafanyakazi afya walisema.
Waasi wa Kihouthi wa Yemen Jumapili walisema walishambulia meli mbili za kiraia, na moja ya kivita ya Marekani katika Bahari ya Sham na Bahari ya Arabia, katika juhudi zao za hivi karibuni kuzorotesha safari za meli katika kile wanachosema ni kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza.
Rais wa Nigeria Bola Tunubu amesema Jumatano kwamba mageuzi ya kiuchumi yataendelea licha ya hali ya maisha kuendelea kuwa ngumu na kusababisha hasira kutoka kwa wananchi, na ameahidi kuwasilisha mswada wa sheria katika bunge hivi karibuni kwa ajili ya kuweka kiwango cha mshahara wa chini.
Shughuli za kutafuta na za uokoaji zitaendelea hadi ndege iliyopotea iliyokuwa inambeba makamu rais wa Malawi Saulos Klaus Chilima, ipatikane, rais wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika alisema Jumatatu.
Mahakama ya rufaa katika jimbo la Georgia Jumatano ilisitisha kwa muda, kesi ya jinai inayomtuhumu Donald Trump kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020, huku ikizingatia ombi la rais huyo wa zamani la kumuondoa mwendesha mkuu Fani Willis katika usimamizi wa kesi hiyo.
Baraza la Wawakilishi la Marekani linaongozwa na Warepublican Jumanne limepitisha mswada ambao utaiwekea vikwazo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa uamuzi wa Mwendesha mashtaka wake mkuu kutaka zitolewe hati za kimataifa za kuwakamata maafisa wa Israel wanaohusishwa na vita huko Gaza.
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol na viongozi wa nchi za Afrika walikubaliana Jumanne kuimarisha ushirikiano wa biashara na kuzindua "mazungumzo ya madini muhimu" yanayolenga maendeleo endelevu ya rasilimali za bara hilo.
Claudia Sheinbaum alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi nchini Mexico na kuwa rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo, akirithi mradi wa mshauri wake na kiongozi anayeondoka madarakani Andres Manuel Lopez Obrador ambaye hatua zake maarufu za kupambana na umaskini zilimsaidia kupata ushindi.
Donald Trump amesema atakubali kifungo cha nyumbani au kifungo cha jela baada ya jopo la Mahakama ya New York kumkuta na hatia wiki iliyopita katika kesi ya kihistoria, lakini itakuwa vigumu kwa wananchi kukubali hilo.
Helikopta iliyokuwa imembeba rais wa Iran Ebrahim Raisi na waziri wake wa mambo ya nje ilianguka siku ya Jumapili ilipokuwa ikivuka eneo la milima katika ukungu mkubwa, wakati ikirejea kutoka kwenye mpaka na Azerbaijan, afisa mmoja wa Iran aliliambia shirika la habari la Reuters.
Jeshi la Uganda limemkamata kamanda wa kundi la waasi linaloshirikiana na Islamic State ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza vilipuzi, au mabomu, ambayo kundi hilo limetumia kufanya mashambulizi mabaya katika siku za nyuma, jeshi lilisema Jumapili.
Vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) vilizuia jaribio la mapinduzi lililohusisha wapiganaji wa Congo na wa kigeni Jumapili asubuhi, msemaji wa jeshi hilo alisema katika hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni.
Maafisa katika mji wa George nchini Afrika Kusini walisitisha shughuli ya kuwatafuta manusura, na miili zaidi, siku ya Ijumaa katika eneo la jengo lililoporomoka ambapo watu 33 walifariki.
Pandisha zaidi