Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 09:51

Utafutaji wa manusura kwenye jengo lililoporomoka Afrika Kusini wasitishwa


PICHA YA MAKTABA: Waokoaji wakiendelea na shughuli zao kwenye jengo lililoporomoka Afrika Kusini.
PICHA YA MAKTABA: Waokoaji wakiendelea na shughuli zao kwenye jengo lililoporomoka Afrika Kusini.

Maafisa katika mji wa George nchini Afrika Kusini walisitisha shughuli ya kuwatafuta manusura, na miili zaidi, siku ya Ijumaa katika eneo la jengo lililoporomoka ambapo watu 33 walifariki.

Waokoaji na wahudumu wa kujitolea wamekuwa wakipitia vifusi kwa siku 11, baada ya jengo la makazi la ghorofa tano lililokuwa linaendelea kujengwa katika jiji la mashariki mwa Cape Town kuporomoka, na kusababisha wingu la vumbi.

Serikali ya Western Cape ilisema sasa inaamini kuwa watu 62 walikuwa kwenye eneo hilo wakati wa mkasa huo. Watu 29 walinusurika baada ya kuokolewa.

Inaaminika kuwa wahamiaji kutoka nchi jirani za Malawi na Zimbabwe walikuwa wakifanya kazi katika eneo la ujenzi pamoja na raia wa Afrika Kusini.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Malawi amesema raia tisa wa nchi yake wamethibitishwa kufariki katika tukio hilo na 11 wameokolewa. Wawili kati yao wamelazwa hospitalini.

Sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo bado haijajulikana, na uchunguzi unaendelea.

Rais Cyril Ramaphosa alitembelea eneo hilo siku ya Alhamisi na kukutana na familia za waathiriwa.

Forum

XS
SM
MD
LG