Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 07:34

Afrika kusini imetoa wito kwa UN kwamba Israel isitishe mapigano Gaza


Vuzimuzi Madonsela, Balozi wa Afrika kusini nchini Uholanzi
Vuzimuzi Madonsela, Balozi wa Afrika kusini nchini Uholanzi

Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi amelisihi jopo la majaji 15 wa kimataifa kuiamuru Israel iondoke bila masharti huko Gaza.

Afrika Kusini imetoa wito Alhamis kwa mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa kuamuru sitisho la mapigano huko Gaza wakati wa kikao kuhusu hatua za dharura za kusitisha operesheni za kijeshi za Israel katika mji wa kusini wa Rafah.

Hii ni mara ya tatu kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki kufanya vikao vya kusikiliza mgogoro wa Gaza tangu Afrika Kusini ilipofungua kesi mwezi Disemba katika mahakama hiyo, yenye makao yake mjini The Hague nchini Uholanzi, iki-ishutumu Israel kwa mauaji ya kimbari.

Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi, Vusimuzi Madonsela, amelisihi jopo la majaji 15 wa kimataifa kuiamuru Israel “iondoke kabisa bila masharti” kutoka Ukanda wa Gaza. Mahakama hiyo tayari imegundua kuwa kuna “hatari halisi na ya hivi sasa” kwa watu wa Palestina huko Gaza kutokana na operesheni za kijeshi za Israel.

“Hii inaweza kuwa fursa ya mwisho kwa mahakama kuchukua hatua”, alisema wakili wa Ireland, Blinne Ní Ghrálaigh, ambaye ni sehemu ya timu ya sheria ya Afrika Kusini.

Forum

XS
SM
MD
LG