Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:46

Rais wa Tunubu asema Nigeria itaendelea na Mageuzi ya kiuchumi.


Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu (Kushoto) akiwa katika mkutano wa kiuchumi uliofanyika Riyadh Aprili 28, 2024. Picha na Fayez Nureldine / AFP
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu (Kushoto) akiwa katika mkutano wa kiuchumi uliofanyika Riyadh Aprili 28, 2024. Picha na Fayez Nureldine / AFP

Rais wa Nigeria Bola Tunubu amesema Jumatano kwamba mageuzi ya kiuchumi yataendelea licha ya hali ya maisha kuendelea kuwa  ngumu na kusababisha hasira kutoka kwa wananchi, na ameahidi kuwasilisha mswada wa sheria katika bunge hivi karibuni kwa ajili ya kuweka kiwango cha mshahara wa chini.

Tinubu, aliyeingia madarakani mwaka mmoja uliopita aliondoa ruzuku ya miongo kadhaa ya mafuta ambayo ilisababisha bei kuwa chini na kushusha thamani ya sarafu, hatua iliyopelekea ongezeko la mfumuko wa bei kwa asilimia 33 .69 mwezi April, kiwango chake cha juu zaidi katika takriban miongo mitatu na kudidimiza mapato.

Katika hotuba kwa taifa kuadhimisha siku ya demokrasia, Tinubu alikubali kwamba hali ngumu imesababishwa na mageuzi, ambayo pia ni pamoja na viwango vya juu vya riba na kuondolewa kwa sehemu ya ruzuku ya umeme lakini alisema hii itaunda msingi mzuri wa ukuaji wa siku zijazo.

“ninaelewa hali ngumu ya uchumi tunaokabiliana nao kama taifa wakati huu, uchumi wetu umekua ukihitaji mageuzi kwa miongo kadhaa sasa. Mageuzi tuliyoweka yana lengo la kuimarisha msingi bora kwa ajili ya ukuaji wa siku za mbele” alisema rais huyo wa Nigeria.

Forum

XS
SM
MD
LG