Muungano mkubwa wa vyama vya wafanyakazi nchini Nigeria ilitangaza mgomo kuanzia leo Jumatatu, baada ya kushindwa kukubaliana na serikali kuhusu kiwango cha chini cha malipo kinachostahili kutolewa kwa wafanyakazi.
Nigeria labour congress NLC na Trade union congress TUC vilitangaza mnamo Mei tarehe 1 kwamba wanachama wake wataanza mgomo iwapo makubaliano kuhusu kiwango cha chini cha mshahara yatakuwa hayajafikiwa kufikia mwishoni mwa mwezi.
Wametangaza mgomo kwa muda usiojulikana baada ya mazungumzo kukwama na wamesisitiza kwamba mgomo utaendelea hadi serikali itakapoweka kiwango kipya cha chini cha mshahara wa wafanyakazi.
Forum