Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:38

Nigeria katika giza, safari za ndege zimesitishwa


Wafanyakazi wanaogoma nchini Nigeria
Wafanyakazi wanaogoma nchini Nigeria

Miungano mikubwa ya vyama vya wafanyakazi nchini Nigeria imezima mitambo ya kuzalisha umeme na kuathiri usafiri wa ndege kote nchini, katika siku ya kwanza ya mgomo unaosababishwa na hatua ya serikali kutoweka kima cha chini cha mishahara.

Mgomo huo wanne tangu rais Bola Tinubu alipoingia madarakani, unaongozwa na muungano wa wafanyakazi wa Nigeria Labour Congress NLC na Trade Union Congress TUC.

Shirika la kusambaza umeme Nigeria TCN, limesema kwamba wanachama wake waliwafukuza wafanyakazi katika vyumba vilivyo na mitambo ya kusambaza umeme na wameanza kwa kufunga vituo sita kabla ya kufunga mfumo mzima wa kusambaza umeme saa nane dakika 19 usiku, kwa saa za Nigeria.

Shirika la ndege la Nigeria Ibom Air, limetangaza kusitisha safari za ndege kwa muda usiojulikana kutokana na mgomo, huku shirika la United Nigeria likisema viwanja vote vya ndege kote nchini humo vimefungwa na wafanyakazi wanaogoma wamezuia safari za ndege.

Forum

XS
SM
MD
LG