Moshi ulikuwa umesambaa katika eneo la mpakani la kaskazini mwa Israel Alhamisi (Mei 16) baada ya msururu wa makombora kufyatuliwa kutoka Lebanon na kupiga maeneo ambayo hayana watu, huku Hezbollah ikiwa inafanya mashambulizi kwa kutumia droni na makombora yanayopigwa bila ya shabaha.
Kikundi cha Wafilipino kinachoongoza juhudi ya kusambaza mahitaji muhimu katika Bahari ya South China kimefikisha chakula na mafuta kwa wavuvi wa Ufilipino licha ya kufuatiliwa na vyombo vya majini vya China, maafisa wake walisema Alhamisi, wakiita ni “ushindi mkubwa.”
Jeshi la Israel Jumanne (Mei 14) lilitoa kanda ya video iliyochukuliwa na droni ikiwaonyesha watu wenye silaha wakiwa wamesimama pembeni ya gari lililokuwa na nembo ya UN katika eneo la Umoja wa Mataifa huko kusini mwa Gaza, katika mji wa Rafah, na wameutaka Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi.
Idadi ya Raia wanaokufa inaendelea kuongezeka wakati Israel ikiwa imezidisha mashambulizi upande wa kaskazini na kusini mwa Gaza siku ya Jumatatu.
Majeshi ya Israeli yamerejea kuendeleza mapigano upande wa kaskazini wa Ukanda wa Gaza.
Milipuko mikubwa ya mabomu inayotokana na mashambulizi ya anga na mizinga iliyorushwa iliutikisa upande wa kaskazini mwa Gaza kuanzia Jumamosi (Mei 11), moshi uliokuwa ukitoka katika majengo ulionekana kutoka Israel huku mapigano kati ya Israel na Hamas yakiendelea.
Walinzi wa Pwani wa Ufilipino (PCG) wameazimia kuendeleza uwepo wao katika eneo lenye mzozo la bahari ya South China Sea kuhakikisha kuwa China haitekelezi harakati zake za kurejesha eneo la Sabina Shoal, msemaji wake alisema Jumatatu (Mei 13).
Watu saba waliuawa na wengine 17 kujeruhiwa wakati sehemu nzima ya jengo la ghorofa huko Russia iliporomoka baada ya kushambuliwa na kombora la enzi ya Sovieti lililorushwa na Ukraine na kutunguliwa na Russia, maafisa walisema.
Vifaru vya Israel vimeingia ndani upande wa mashariki katika mji wa Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mapema Jumapili, baada ya usiku wa mashambulizi makali ya anga na ardhini, na kuua watu 19 na kujeruhi wengine kadhaa, maafisa wa afya wamesema.
Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika jimbo la Brazil la Rio Grande do Sul imeongezeka hadi 136, kitengo cha ulinzi wa raia katika eneo hilo kilisema Jumamosi, kutoka idadi ya awali ya 126 , huku watu wengine 125 wakiwa hawajulikani walipo.
Kuvurugika kwa misafara ya meli za mizigo katika Bahari ya Sham kumeongezeka na inatarajiwa kupunguza uwezo wa sekta hiyo kati ya nchi za Mashariki ya Mbali na Ulaya kwa kiasi cha asilimia 15 -20 katika robo ya pili ya mwaka, kikundi cha usafirishaji cha Maersk kilisema Jumatatu.
Takriban wahamiaji 107 wakiwemo wanawake na watoto wameachiliwa kutoka kizuizini katika mji ulioko kusini mashariki mwa Libya, msemaji wa kikosi cha usalama alisema Jumatatu.
Shambulio la anga la Israel Jumapili liliua watu wanne wa familia moja katika nyumba kwenye kijiji cha mpakani kusini mwa Lebanon, vyanzo vya ulinzi na usalama wa raia vimesema.
Uturuki haitafanya tena biashara na Israel yenye thamani ya dola bilioni 7 kwa mwaka hadi litakapopatikana sitisho la mapigano la kudumu huko Gaza na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia Wapaletina bila ya kizuizi, waziri wa biashara wa Uturuki amesema leo Ijumaa.
Wanajeshi wa Russia wameingia kambi ya jeshi la anga nchini Niger ambayo ilikuwa inatumiwa na wanajeshi wa Marekani, afisa mkuu wa jeshi la Marekani ameliambia shirika la habari la Reuters, hatua inayofuatia uamuzi wa utawala wa kijeshi wa Niger kuwafukuza wanajeshi wa Marekani.
Mahakama kuu nchini Ghana imefuta mashitaka kwa Rais Nana Akufo-Addo ya kushindwa kuchukua hatua za haraka kuhusiana na mswaada unaopinga Ushoga (LGBTQ) iliyopitishwa na Bunge mwezi Februari, ilitua hukumu hiyo Jumatatu.
Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways Jumatatu limesema litasitisha safari za ndege kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kinshasa, baada ya mamlaka ya kijeshi kushindwa kuwaachilia wafanyakazi wake inaowazuia licha ya amri ya mahakama.
Watu 42 wamefariki katika mafuriko katika eneo la Mai Mahiu katikati mwa Kenya baada ya bwawa kupasuka mapema Jumatatu, na idadi ya vifo inaweza kuongezeka, polisi wamesema.
Mahakama ya mapinduzi ya Iran imemhukumu kifo mwanamuziki maarufu wa Iran Toomaj Salehi kwa mashtaka yanayohusiana na maandamano ya 2022-2023, wakili wake ameliambia gazeti la Iran la Sharq Jumatano.
Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Soussa Jumanne alisema nchi yake iliwajibika kwa uhalifu uliofanywa wakati wa enzi ya utumwa na ukoloni, na amesema kuna haja ya kulipa fidia.
Pandisha zaidi