Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:16

Uturuki yasitisha biashara na Israel hadi kupatikane sitisho la mapigano Gaza


Waziri wa biashara wa Uturuki Omer Bolat
Waziri wa biashara wa Uturuki Omer Bolat

Uturuki haitafanya tena biashara na Israel yenye thamani ya dola bilioni 7 kwa mwaka hadi litakapopatikana sitisho la mapigano la kudumu huko Gaza na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia Wapaletina bila ya kizuizi, waziri wa biashara wa Uturuki amesema leo Ijumaa.

Mwenendo wa Israel wa kutotaka kufikia makubaliano na hali inayozidi kuwa mbaya huko Gaza imepelekea Uturuki kusitisha biashara, Omar Bolat amesema katika hotuba yake mjini Istanbul, wakati akitangaza takwimu za biashara za mwezi Aprili.

Uamuzi wa Uturuki ambao ulitangazwa Alhamisi, umekuwa wa kwanza kwa mshirika huyo mkuu wa biashara wa Israel kusitisha mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa kutokana na operesheni za kijeshi huko Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Katz ameikosoa hatua ya Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, akisema inavunja makubaliano ya kimataifa ya biashara na hiyo ndiyo “tabia ya dikteta”.

Kundi la Hamas linalodhibiti Gaza, limepongeza uamuzi huo kuwa wa kijasiri na unaounga mkono haki za Wapalestina.

Forum

XS
SM
MD
LG