Maandamano ya wanaounga mkono Wapalestina yameongezeka katika vyuo vikuu vya juu vya Marekani siku ya Jumatatu.
Maafisa wawili wa ngazi ya juu wa Uingereza Jumanne wameomba serikali ifikirie tena mpango wake wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda, wakionya kuwa hatua hiyo huenda ikawa ni matokeo mabaya kwa haki za kibinadamu pamoja na usalama wa wakimbizi.
Qatar inafikiria tena jukumu lake kama mpatanishi kati ya Israel na Hamas, waziri mkuu amesema jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Doha akiwa na mwenzake wa uturuki.
Kombora la Russia Jumatano liliua wakazi 9 na kuharibu majengo na miundombinu ya mji wa kaskazini mwa Ukraine wa Chernihiv, maafisa wa mji huo walisema.
Kundi la mataifa yanayozalisha mafuta la OPEC+, baada ya kupoteza uanachama wa Angola miongoni mwa wengine katika miaka ya karibuni sasa linalenga kuikaribisha Namibia kujiunga nalo
Idara ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria imesema kuwa tayari imepata karibu dola milioni 27 kufuatia uchunguzi dhidi ya waziri wa serikali aliyesimamishwa kazi, pamoja na maafisa wengine.
Takriban watu 12 waliuawa na zaidi ya 50 bado hawajulikani walipo, baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi kwenye mto kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa eneo hilo, na kiongozi wa shirika la kiraia walisema Jumapili.
Thailand imetuma ujumbe kwa utawala wa kijeshi Myanmar ili kupunguza ghasia, waziri wake wa mambo ya nje amesema leo.
Wanajeshi wa Israel wamewapiga risasi wapalestina wawili mapema leo karibu na Ukingo wa Magharibi katika mji wa Tubas, vyombo vya habari vya Palestina na Israel vimeripoti.
Vyama vya siasa na mashirika ya kiraia nchini Mali Alhamisi yametupilia mbali kwa pamoja amri ya utawala wa kijeshi ya kusimamisha shughuli za kisiasa na yameapa kuweka pingamizi ya kisheria dhidi ya kile mwanasiasa mmoja wa upinzani amekitaja kuwa “hatua ya kidikteta.
Nyota wa zamani wa Ligi ya Mpira wa Marekani NFL na mcheza filamu ambaye alifutiwa mashtaka ya mauaji ya mkewe na rafiki yake wa kiume katika kesi iliyoteka Marekani na dunia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, na Rais wa Rwanda Paul Kagame, wamesema wanatazamia safari za ndege, chini ya mpango wa Uingereza wa kuwahamishia waomba hifadhi nchini Rwanda zitaanza majira ya machipuko yani Spring.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano haraka iwezekanavyo nchini Ukraine.
Wanawake wazee Nchini Uswizi walisherehekea ushindi wao wa "kihistoria" katika uamuzi wa kipekee kuhusu hali ya hewa kutoka Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) Jumanne.
Taifa la Nicaragua Jumatatu Limetoa wito kwa Mahakama ya Juu ya Umoja wa Mataifa kusitisha misaada wa kijeshi ya Ujerumani na misaada mingine kwa Israel.
Ujumbe wa Hamas uliwasili mjini Cairo kukutana na mkuu wa idara ya ujasusi ya Misri Abbas Kamel, taarifa ya kundi la Hamas ilisema Jumapili.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amewasili Guangzhou leo Alhamisi kuanzia ziara ya ufuatiliaji huko China ikiwa ni chini yam waka mmoja.
Spika wa Bunge la Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula alisema Jumatano kwamba anajiuzulu wadhifa wake huku kukiwa na uchunguzi wa tuhuma za rushwa wakati akiwa waziri wa ulinzi.
Waandamanaji wanaoipinga serikali wanakusanyika nje ya Bunge la Israel mjini Jerusalem na kuandamana hadi kwenye makazi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, wakitaka uchaguzi wa mapema na makubaliano ya kutekwa nyara huku kukiwa na hasira juu ya jinsi vita vya Gaza vilivyoshughulikiwa.
Pandisha zaidi