Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 14, 2024 Local time: 09:44

Qatar yafikiria iwapo iendelee na jukumu la usuluhishi kati ya Israel na Hamas


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kulia) na Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al Thani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kulia) na Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al Thani

Qatar  inafikiria tena jukumu lake kama mpatanishi kati ya Israel na Hamas, waziri mkuu amesema jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Doha akiwa na mwenzake  wa uturuki.

Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani amesema upatanishi wake umekuwa ukichukuliwa vibaya, bila ya kufafanua.

Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, Waziri Mkuu wa Qatar anasema: “Suala hili limechukua miezi mingi, na tofauti zimekuwa zikiongezeka. Siku zote tumefanya kazi kwa karibu na washirika wetu katika upatanishi, Marekani na Misri, ili kuziba mwanya na kuwasilisha mapendekezo kulingana na hayo.

Israel ikishambulia kijiji cha Khiam kusini mwa Lebanon April 17, 2024, wakati mvutano kati ya mpaka wa nchi hizo mbili ukiendelea huku mapigano kati ya Isreal na wanamgambo wa Hamas yakijiri huko Ukanda wa Gaza. (Photo by Rabih DAHER / AFP)
An Israeli strike illuminates the sky above the southern Lebanese village of Khiam late on April 17, 2024.

Hata hivyo, mwishowe, jukumu la upatanishi limekuwa dogo, nina maana, lina viwango vyake na haliwezi kukidhi. Pande husika zinakataa.”

Qatar, Misri na Marekani wamehusika katika mazungumzo ya kufaniksiha kupatikana kwa sitisho la mapigano ambalo litajumuisha kuachiliwa kwa baadhi ya mateka ambao wanaendelea kushikiliwa na Hamas huko Gaza na Israel kuwaachia wafungwa wa Kipalestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alijadilia suala hilo kwa njia ya simu ya Waziri Mkuu wa Qatar siku ya Jumanne.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema maafisa wawili wamethibitisha “umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa karibu pamoja na katika siku za usoni kufanikisha sitisho la mapigano huko Gaza ambalo litapelekea kuachiliwa kwa mateka.”.

Forum

XS
SM
MD
LG