Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:11

White House yaipongeza Israel kuzuia mashambulizi ya Iran


Msemaji wa masuala ya usalama wa taifa wa White House, John Kirby, amesema Marekani na washirika wengine wanaona yalikuwa ni mafanikio ya makubwa ya kijeshi ya Israel, katika kuzima mashambulizi ya zaidi ya ndege zisizo na rubani 300 na makombora yaliyorushwa na Iran.

Kirby alipokuwa kwenye televisheni za CNN, na NBC, Jumapili asubuhi amesema dazeni kadhaa ya ndege zisizo na rubani na makombora zilizolenga Israel, lakini zilitunguliwa na jeshi la Marekani.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, katika taarifa yake Jumamosi jioni, alisema ndege na makombora hayo yalirushwa kutoka maeneo ya Iran, Iraq, Syria na Yemen.

“Tunatoa wito kwa Iran, kusimamisha mara moja mashambulizi mengine, pia ya vikosi vyake vya ushirika ili kupunguza mvutano,” mkuu wa ulinzi wa Marekani, alisema.

Amesisitiza hawataki mzozo na Iran, lakini hawatasita kulinda vikosi vyake na kusaidia ulinzi kwa Israe.

Forum

XS
SM
MD
LG