Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:08

Israel imezuia mashambulizi ya Iran


Israel, Jumapili imesema Iran ilifanya mashambulizi ya makombora 320 ya kivita dhidi yake katika shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa, lakini ulinzi wake wa anga pamoja na Marekani na nchi nyingine zinazoiunga mkono uliyatungua kwa asilimia 99.

Msemaji wa jeshi la ulinzi la Israel (IDF), Luteni kanali Peter Lerner, aliiambia CNN kwamba Iran, ilishindwa katika mashambulizi yao.

Lerner amesema Tehran, ililenga kambi ya kijeshi ambayo Iran, inasema ilitumiwa kufanya shambulizi la Aprili 1 kwenye ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus, na kuwaua majenerali wawili wa Iran.

Alisema shambulio la anga la usiku halikusababisha uharibifu mkubwa. Msemaji huyo wa IDF amesema Iran, ilirusha ndege zisizo na rubani 170, makombora 120 na 30 ya baharini, huku mengi yao yakitoka moja kwa moja katika ardhi ya Iran ingawa baadhi yalirushwa na wanamgambo washirika wa Iran, waliopo Iraq na Yemen.

Forum

XS
SM
MD
LG