Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 14, 2024 Local time: 20:23

Moscow yakwepa kulaani shambulizi lililofanywa na Iran dhidi ya Israel


 Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Moscow imekwepa kulaani shambulizi la Iran dhidi ya Israel wakati ikiwataka viongozi wa Israel kujizuia.

Wachambuzi wanasema taarifa za Kremlin zinaonyesha zimeichagua Iran kama mshirika wanayempenda na kuaacha uwiano wa kidiplomasia katika masuala nyeti ambayo yamekuwa yakijitokeza katika eneo hilo.

Kremlin ilijibu shambulizi la Iran kwa Israel kwa mchanganyiko wa diplomasia na kulipiza kisasi. Msemaji wa Rais Vladimir Putin, Dmitri Peskov alitoa taarifa kwa njia ya simu na kuripotiwa na shirika la habari la Reuters.

Dmitri Peskov, Msemaji wa Kremlin alisema: “Tuna wasiwasi mkubwa sana kuhusu kusambaa kwa mivutano katika eneo hilo. tunazitaka nchi zote katika eneo hilo kujaribu kujizuia. “

Dmitri Peskov
Dmitri Peskov

Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa Vasily Nebenzya ametoa taarifa kali, ambayo inaweka jukumu la uwajibikaji kwa kuongezeka tena kwa mvutano kati ya Israel na Magharibi.

Vasily Nebenzya, Mwakilishi wa Russia UN alisema: “Tunaona ishara zilizowekwa na Tehran kwamba hawataki kusambaa zaidi kwa mivutano ya kijeshi dhidi ya Israel, na tunaisihi Magharibi na Jerusalem kufanya hivyo hivyo na kukataa kutumia nguvu huko Mashariki ya Kati.”

Katika maelezo yaliyobandikwa kwenye mtandao wa kijamii, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova amekosoa matarajio yoyote kwamba Russia huenda ikailaani Iran kwa shambulizi, wakati Israel, amesema, haijakosoa mashambulizi ya Ukraine kwenye eneo la Russia.

Maria Zakharova
Maria Zakharova

Israel imelaani uvamizi kamili wa Russia kwa Ukraine.

Wachambuzi wanasema vita nchini Ukraine vimepelekea Moscow kuacha kile walichokuwa wanakielezea hapo awali kuwa ni msimamo wa kadri huko Mashariki ya Kati, na hivi sasa kuamua kuonyesha uungaji mkono wa wazi kwa Tehran.

James Nixey, Chatham House anasema: “Ukweli ni kwamba Moscow kwa makini sana inadhibiti na inasawazisha uhusiano na mataifa yote ya Mashariki ya kati hivi sasa. Sababu ya kubadilika ni kutokana na muktadhan wa vita nchini Ukraine, ambapo Russia inataka kile inachokitaka, inahitaji kile inachohitaji na iko tayari kujitoa katika uhusiano ili kuendelea lile inalolitaka.”

Kama waangalizi wanavyoona, Russia inaonekana kuunga mkono makabiliano ya Mashariki ya Kati, kuashiria kuongezeka kwa athari za uvamizi wake kamili nchini Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG