Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:35

Kikosi malumu cha Iran, chavamia meli yenye uhusiano na Israel


Wanakikosi maalumu cha jeshi maalumu la Kimapinduzi la Iran, walishuka kutoka kwenye helikopta kuingia katika meli ya makasha yenye uhusiano na Israel, karibu na mlango wa bahari wa Hormuz na kuikamata meli hiyo Jumamosi.

Hili linakuwa ni shambulizi la karibuni kabisa baina ya nchi hizo mbili.

Mashariki ya Kati imekuwa ikijiandaa na uwezekano wa ulipiziwaji kisasi wa Iran, kutokana na shambulizi linaloshukiwa kufanywa na Israel, mapema mwezi huu katika ubalozi mdogo wa Iran, wa Syria na kusababisha vifo vya watu 12, akiwemo jenerali mkuu wa walinzi ambaye aliwahi kukiongoza kikosi hicho.

Vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza vimefikia mwezi wa sita na vinazidisha mvutano wa miongo kadhaa katika eneo zima.

Shirika la habari la serikali ya Iran, IRNA linasema kikosi maalum cha jeshi la wanamaji la ndicho kimevamia meli hiyo yenye bendera ya Ureno, ya MSC Aries, ikiwa na ushirikiano la kampuni ya meli ya London, Zodiac.

Forum

XS
SM
MD
LG