Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 02:54

Iran yasema balozi za Israel hazipo salama tena


Mshauri wa kiongozi mkuu wa Iran, Jumapili ameonya kwamba balozi za Israel, haziko tena salama baada ya shambulizi nchini  Syria, ambalo Tehran, imeilaumu Israel, kuwaua maafisa saba wa ulinzi wa Kimapinduzi.

“Balozi za utawala wa Kizayuni haziko tena salama,” Yahya Rahim Safavi, mshauri mkuu wa Ayatollah Ali Khamenei, alinukuliwa na shirika la habari la ISNA, akisema hayo.

Tehran imeapa kulipiza kisasi shambulizi la anga la Jumatatu dhidi ya Damascus, ambalo liliharibu ubalozi mdogo wa Iran na kuua maafisa saba wa jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wakiwemo majenerali wawili.

“Upinzani upo tayari na tusubiri kuona namna litakavyo jibiwa,” Safavi amesema akibainisha kuwa kukabiliana na utawala huu katili ni haki ya kisheria na ina uhalali.

Pia alibainisha kufungwa kwa balozi nyingi za Israeli, kuzunguka eneo hilo. Hakuna majibu kutoka Israeli, kuhusiana na suala hili.

Forum

XS
SM
MD
LG