Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 14, 2024 Local time: 20:35

Israel imetoa wito wa vikwazo vipya dhidi ya Iran


Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Israel Katz
Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Israel Katz

Waziri wa mambo ya nje wa Israel amesema amewasiliana na mataifa zaidi ya 30 kushinikiza vikwazo dhidi ya mpango wa makombora wa Iran.

Israel imetoa wito wa vikwazo vipya dhidi ya Iran kama sehemu ya majibu kwa jeshi la Iran na baadhi ya washirika wake kuanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Israel Katz amesema katika mitandao ya kijamii kwamba amewasiliana na mataifa zaidi ya 30 kushinikiza vikwazo dhidi ya mpango wa makombora wa Iran na kwa kutangaza kuwa jeshi la Iran la Revolutionary Guard Corps (IRGC) ni kundi la kigaidi.

Marekani ni moja ya nchi kadhaa ambazo tayari zimeitaja IRGC kama kundi la kigaidi. Tangu mwezi Oktoba, Marekani imeweka vikwazo kadhaa vinavyolenga mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran wakati vikwazo vya Umoja wa Mataifa vikimalizika.

Israel pia inaonekana kuwa na nia ya kulipiza kisasi kijeshi licha ya wito wa viongozi wa dunia wa kutaka kukomeshwa kwa hali hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG