Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:23

Waziri wa Fedha wa Marekani Aanza Ziara China

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen, kushoto, akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini China Nicolas Burns wakati naibu Waziri wa Fedha wa China Liao Min akimlaki pia, katika Uwanja wa Ndege wa Guangzhou Baiyun kusini mwa Jimbo la Guangdong, China, April 4, 2024.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amewasili Guangzhou leo Alhamisi kuanzia ziara ya ufuatiliaji huko China ikiwa ni chini yam waka mmoja.

Yellen amekwenda Guangzhou na Beijing kwa mikutano na viongozi wa fedha na maafisa wa serikali.

Shughuli zake huko zitahusisha kukutana na Makamu Waziri Mkuu He Lifeng, Gavana wa Benki Kuu Pan Gognsheng, makamu Waziri Mkuu wa zamani Liu He.

FILE — Waziri wa Fedha Janet Yellen, kulia, akiwa na makamu waziri mkuu wa China He Lifeng, walipokutana Nov. 10, 2023, huko San Francisco, California.
FILE — Waziri wa Fedha Janet Yellen, kulia, akiwa na makamu waziri mkuu wa China He Lifeng, walipokutana Nov. 10, 2023, huko San Francisco, California.

Pia atakutana na viongozi wa biashara wa Marekani wanaofanya shughuli zao nchini China, wanafunzi wa chuo kikuu na viongozi wa kieneo.

Kuna mivutano juu ya serikali ya China kuunga mkono uzalishaji wa magari ya umeme na paneli za jua, wakati serikali ya Marekani ikizidisha misaada yake kwa wale walio kwenye sekta za teknolojia.

Forum

XS
SM
MD
LG