Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:10

Rais Biden kukutana na Rais Xi Jinping wa China


Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) na rais wa China Xi Jinping (Kushoto) huko Beijing Agosti 18, 2011. Picha na REUTERS/Lintao Zhang/Pool
Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) na rais wa China Xi Jinping (Kushoto) huko Beijing Agosti 18, 2011. Picha na REUTERS/Lintao Zhang/Pool

Kurejeshwa mawasiliano ya kijeshi kati ya mataifa mawili makubwa duniani litakuwa ajenda kuu ya Rais Joe Biden siku ya Jumatano wakati wa mkutano unaotarajiwa kwa hamu na rais wa China, Xi Jinping, utakaofanyika katika eneo la San Francisco Bay, afisa mkuu wa utawala amesema.

Viongozi hao watakutana pembeni ya mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki ambapo Marekani ni mwenyeji wa mkutano huo.

Mkutano kati ya Biden na Xi utakuwa ni mkutano wa kwanza wa ana kwa ana, kati ya marais hao wawili tangu wakutane mwaka jana mjini Bali, Indonesia.

Utawala wa Biden tayari umeshatuma maafisa kadhaa wa ngazi ya juu kwenda Beijing mwaka huu, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Antony J. Blinken, Waziri wa Fedha Janet L. Yellen na Waziri wa Biashara Gina Raimondo.

Biden "amedhamiria kuchukua hatua muhimu" kuanzisha tena njia za mawasiliano za kijeshi na Beijing, alisema afisa mkuu wa utawala, ambaye alizungumza na waandishi wa habari Alhamisi jioni kwa sharti la kutotajwa jina.

Utawala unaamini kuwa hatua hiyo italeta utulivu zaidi katika uhusiano na kupunguza hatari za makosa ya kijeshi.

China ilisitisha mawasiliano ya kijeshi mwaka jana kupinga ziara ya Spika wa Bunge nchini Taiwan wakati huo alikuwa Nancy Pelosi. Mawasiliano hayo yaliyojumuisha kusimamishwa kwa mazungumzo ya Kuratibu Sera ya Ulinzi, yaliyokusudiwa kudumisha njia bora za mawasiliano na kupunguza hatari, pamoja na Makubaliano ya Mawasiliano ya Kijeshi ya Baharini, ambayo huwawezesha waendeshaji meli na ndege kuwasiliana mara kwa mara.

Blinken hakuweza kuanzisha upya njia za mawasiliano wakati wa ziara yake mjini Beijing mwezi Juni. “Wachina wamekuwa wakisita. Na hivyo, rais atashikiza kwa ujasiri wiki ijayo," afisa mkuu wa utawala alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG