Vyombo vya habari vimesema mwanamme mmoja ameuwawa wakati wanajeshi wa Israel walipolishambulia kwa risasi gari lake huko Tubas. Mpalestina mwingine alipigwa risasi na kuuwawa katika operesheni za kijeshi , kwenye kambi ya wakimbizi ya al Far’a, kusini mwa Tubas.
Hata hivyo jeshi la Israel halijasema lolote kuhusu ripoti hiyo.
Katika tukio tofauti msemaji wa shirika la kuhudumia watoto duniani – UNICEF leo ametoa taarifa inayoonyesha hatari wanazokabiliwa wafanyakazi wa misaada huko Gaza na kueleza kuhusu kuvunjika moyo kutokana na hali inayowakumba wengi katika eneo la vita.
Msemaji wa UNICEF Tess Ingram anakumbuka stori yake ya bahati ya kufanikiwa kutoroka baada ya gari alilokuwa akisafiri nalo lilipolengwa na silaha wakati likisubiri kuingia kaskazini mwa Gaza.
Tukio hilo limetokea karibu na kituo cha ukaguzi cha Wadi huko Gaza, ambako wafanyakazi wa misaada wameelekezwa kusubiri kabla ya kuendelea , kwa mujibu wa Ingram.
Tess Ingram, msemaji wa UNICEF anaeleza :
“Nilikuwa ndani ya gari hilo liliposhambuliwa. Lilikuwa linasubiri kwenye kituo cha ukaguzi kusini mwa Wadi Gaza, ambako mara nyingi tunaelekezwa kusubiri kabla ya kuitwa kwenye ukaguzi. Tulikuwa tunasubiri pale kama tulivyoelekezwa, na milio ya risasi ikazuka katika eneo hilo. ilionekana kutoka kwenye kituo cha ukaguzi kuelekea kwa raia ambao walikimbia kuondoka katika kituo cha ukaguzi. Kwa bahati nzuri mimi na wafanyakazi wenzangu sote tulikuwa salama.
Forum