Katika taarifa ya pamoja, Fillippo Grandi kamishna wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, na Volker Turk kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja huo, wameishauri Uingereza badala yake ishughulikie wimbi la wahamiaji na wakimbizi wanaoingia nchini humo.
Grandi amesema kuwa sheria mpya ya Uingereza inakwenda kinyume na utamaduni wake wa kutoa hifadhi kwa wanaohitaji, ikikiuka mkataba wa kimataifa wa wakimbizi. Turk awali alilalamikia mpango huo amesema kuwa unahujumu utawala wa sheria wa Uingereza na mfano mbaya kwa ulimwengu.
Jumatatu waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak aliahidi kuanza kupeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ndani ya kati ya wiki 10 hadi 12 zijazo.
Forum