Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 12:02

Waziri Mkuu wa Uingereza aahidi kuwarejesha wakimbizi nchini Rwanda


Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak akizungumza na waandishi wa habari mjini London. April 22, 2024.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak akizungumza na waandishi wa habari mjini London. April 22, 2024.

Sunak alisema serikali imekodisha  ndege za kibiashara na imewapatia mafunzo wafanyakazi ili kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameahidi leo Jumatatu kuanza kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ndani ya wiki 10 hadi 12, akiliambia bunge kwamba atailazimisha sheria hiyo mpya kupita licha ya upinzani uliopo.

Sunak alisema serikali imekodisha ndege za kibiashara na imewapatia mafunzo wafanyakazi ili kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, ikiwa ni sehemu ya sera anayotarajia itakiimarisha chama chake cha Conservative kabla ya uchaguzi baadaye mwaka huu. Hakuna kama, au lakini, ndege hizi zinakwenda Rwanda, Sunak aliwaambia waandishi wa habari.

Maelfu ya wahamiaji wengi wakikimbia vita na umaskini barani Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, wamewasili Uingereza katika miaka ya hivi karibuni, hasa kwa kuvuka njia ya bahari kwa kutumia boti ndogo katika safari hatari zilizoandaliwa na magenge ya yanayofanya magendo ya kusafirisha watu.

Forum

XS
SM
MD
LG