Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Congress nchini India Rahul Gandhi aliwasilisha uteuzi wake kwa uchaguzi mkuu ujao kutoka eneo bunge la Wayanad kusini leo Jumatano .
Madkatari kutoka hospitali za umma nchini Kenya ambao wamekuwa kwenye mgomo wa kitaifa tangu mwezi uliopita, Jumanne wamekusanyika kwenye miji mwili mikubwa, ili kushauriana kuhusu malalamiko yao dhidi ya serikali.
Darzani za maelfu ya Waisraeli Jumapili walikusanyika nje ya jengo la bunge mjini Jerusalem katika maandamano makubwa Zaidi ya kuipinga serikali tangu nchi hiyo ilipoingia vitani mwezi Oktoba mwaka jana.
Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameahidi kupambana na ufisadi ndani ya jeshi baada ya kuchukua usukani kama kamanda wa juu, hatua inayoonekana kwa kiasi kikubwa kuharakisha hatua ya kuelekea kumrithi baba yake.
Rais wa Russia Vladimir Putin amewaonya washirika wa Ukraine, mataifa ya Magharibi, dhidi ya kutoa msaada wa vituo vya anga katika nchi zao.
Kiwanda cha kusafisa mafuta cha Dangote huenda kikafikisha kikomo biashara ya mafuta ya miaka mingi kutoka Ulaya hadi Afrika, yenye thamani ya dola bilioni 17 kila mwaka, huku viwanda wa Ulaya vikiwa kwenye hatari ya kufungwa kutokana na ushindani mkubwa uliopo, wachambuzi wanasema.
Mahakama moja ya Tunisia Jumatano imetoa hukumu ya kifo kwa watu wanne, na wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha maisha, baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mwanasiasa mashuhuri Chokri Belaid miaka 11 iliyopita, yakiwa mauaji ya kwanza ya kisiasa nchini humo ndani ya miongo kadhaa.
Kundi la Hamas Jumatatu liliwambia wapatanishi kwamba litaendelea kushikilia msimamo wake wa awali kuhusu kufikia makubaliano ya sitisho la mapigano la kudumu, ikiwemo kuwaondoa wanajeshi wa Israel ndani ya Gaza na kurejea nyumbani kwa Wapalestina waliyolazimishwa kuhama makazi yao.
Shinikizo zaidi linaendelea kutolewa kwa Taifa la Israel kusitisha vita kufuatia makubaliano ya kimataifa yaliyojadiliwa Jordan Jumatatu pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huku wakielezea shambulio dhidi ya Rafah huenda litasababisha maafa ya kibinadamu.
Hesabu za kwanza katika vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa rais uliocheleweshwa nchini Senegal Jumapili zinaonyesha mgombea wa upinzani Bassirou Diomaye Faye akiongoza.
Spika wa Bunge la Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula, alisema Alhamisi kwamba atachukua likizo maalum, kutokana na uchunguzi wa tuhuma za rushwa, wakati alipokuwa waziri wa ulinzi.
Russia imefanya shambulio lake kubwa zaidi la kombora katika wiki kadhaa huko Kyiv na eneo linaloizunguuka leo na kujeruhi takriban watu 17 na kuharibu shule , majengo ya makazi na majengo ya viwanda , maafisa wamesema.
Takriban maafisa 70 wa zamani wa Marekani, wanadiplomasia na maafisa wa jeshi Jumatano walimtaka Rais Joe Biden kuionya Israel kuhusu kukabiliwa na hatua kali ikiwa itawanyima Wapalestina haki zao za kiraia na mahitaji msingi.
Afisa wa ngazi ya juu wa Sudan Kusini amesema Jumatano kwamba vijana waliokuwa wamejihami wameua watu 15 kwenye jimbo la Pibor, akiwemo mkuu wa Kaunti, wakati hali ya taharuki ikiendelea kuongezeka nchini humo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka.
Rais wa Marekani Joe Biden alimuonya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumatatu kwamba mashambulizi ya ardhini katika mji wa Rafah yatakuwa "kosa," walipozungumza kwa mara ya kwanza ndani ya mwezi mmoja, huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kuhusu vita katika Ukanda wa Gaza.
Utawala wa kijeshi nchini Niger umebatilisha mkataba wa kijeshi ambao uliruhusu kuwepo kwa wanajeshi na wafanyakazi wa kiraia kutoka Wizara ya Ulinzi ya Marekani katika ardhi yake, msemaji wa utawala Kanali Amadou Abdramane amesema Jumamosi.
Raia wa Russia walianza kupiga kura leo Ijumaa katika uchaguzi wa rais wa siku tatu unaotarajiwa kumkabidhi kiongozi mwenye msimamo mkali Vladimir Putin muhula mwingine wa miaka sita huku mashambulizi mapya yakiendelea nchini Ukraine hadi katika eneo la Russia.
Rais wa Misri Abdel Fattah al–Sisi amesema Ijumaa kwamba taifa lake linajaribu kufikia makubaliano ya sitisho la mapigano huko Gaza, ili kuongeza misaada kuingia, ili kuwaruhusu watu waliokoseshwa makazi kusini mwa eneo dogo, kuhamia kaskazini.
Kiongozi wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa nchini Senegal Ousamne Sonko na mgombea wa urais anayeunga mkono katika uchaguzi wa Machi 24, Bassirou Diomaye Faye, waliachiwa huru kutoka jela Alhamisi, televisheni ya serikali ya Senegal RTS ilisema kwenye tovuti yake.
Pandisha zaidi