Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:44

Rais wa Misri kufanya kila awezalo kushinikiza sitisho la mapigano la Gaza


Rais wa Misri Fattah al-Sisi
Rais wa Misri Fattah al-Sisi

Rais wa Misri Abdel Fattah al–Sisi amesema  Ijumaa kwamba taifa lake linajaribu kufikia makubaliano ya sitisho la mapigano huko Gaza, ili kuongeza misaada kuingia, ili kuwaruhusu watu waliokoseshwa makazi  kusini mwa eneo dogo, kuhamia kaskazini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Sisi pia ameonya kuhusu hatari ya mashambulizi ya Isreal kwenye mji wa Rafah ambako takriban watu milioni1.5 wamechukua hifadhi, karibu na mpaka kati ya Gaza na Misri. Maafisa wa misaada wameonya kuhusu uwezekano wa baa la njaa kwenye eneo hilo la ukanda wa pwani.

Misri ambayo inahofia ongezeko kubwa la wapalestina wasiokuwa na makazi waliosongamana karibu na mpaka wake, na imekuwa ikijaribu kushauriana na Qatar na Marekani, katika mazungumzo ya kuleta maridhiano kati ya Isreal na Hamas kuelekea sitisho la mapigano, kuachiliwa kwa mateka wa Isreal waliopo Gaza, pamoja na kuachiliwa kwa wafungwa wa kivita wa Palestina waliopo Israel.

Alhamisi wizara ya mambo ya nje ya Maisri imeiomba Israel kufungua mpaka wake na Gaza, ili kuruhusu upelekaji zaidi wa misaada ya kibinadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG