Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:43

Wapalestina 29 wauawa wakisubiri msaada huko Gaza-Wizara ya afya ya Gaza


Wapalestina wakibeba magunia ya unga waliyopora kwenye lori la misaada
Wapalestina wakibeba magunia ya unga waliyopora kwenye lori la misaada

Wapalestina wasiopungua 29 waliuawa Alhamisi wakati wakisubiri msaada katika mashambulizi mawili tofauti ya Israel katika Ukanda wa Gaza, wizara ya afya ya Gaza ilisema.

Baadaye, takriban watu 21 waliuawa na zaidi ya 150 kujeruhiwa kwa risasi za Israel kwenye umati wa watu waliokuwa wakisubiri lori za misaada kwenye makutano ya barabara kaskazini mwa Gaza, wizara ya afya ya Gaza ilisema.

Jeshi la Israel limesema linachunguza matukio yote mawili.

Mzozo wa Gaza umewahamisha kwenye makazi yao watu wengi sana kati ya wakazi milioni 2.3 wa eneo hilo.

Matukio mabaya yametokea wakati wa usambazaji wa misaada huku watu wenye njaa wakihangaika kutafuta chakula.

Forum

XS
SM
MD
LG