Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:59

Katibu Mkuu wa UN asema walio wengi wanataka Israel iache vita


Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari ndani ya shule ya UNRWA katika kambi ya wakimbizi wa Palestina Al-Wehdat , Amman, Jordan, Machi 25, 2024.
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari ndani ya shule ya UNRWA katika kambi ya wakimbizi wa Palestina Al-Wehdat , Amman, Jordan, Machi 25, 2024.

Shinikizo  zaidi linaendelea  kutolewa kwa Taifa la Israel kusitisha vita kufuatia makubaliano ya kimataifa yaliyojadiliwa Jordan Jumatatu pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huku wakielezea shambulio dhidi ya Rafah huenda litasababisha maafa ya kibinadamu.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Guterres alisema," Wanaona makubaliano yanayokua yakiibuka katika jumuiya ya kimataifa kuwaambia Waisraeli kwamba sitisho la vita linahitajika.

Guterres alisema kuna matumaini ya maridhiano yanayoongezeka. Aidha aliongeza kuwa Marekani, Umoja wa Ulaya, na ulimwengu wa Kiislamu, wameieleza Israel kwamba uvamizi wowote wa ardhini huko Rafah unaweza kusababisha janga la kibinadamu.

Guterres pia aliahidi kuendelea kufadhili shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA), ambalo alisema linatoa mwanga katika dunia yenye giza.

Guterres alikuwa Misri kabla ya kusafiri kwenda Jordan kama sehemu ya ziara ya kila mwaka ya Mfungo wa mwezi Ramadhani katika nchi za Kiislamu.

Alisafiri siku ya Jumamosi hadi kwenye mpaka wa Misri na Gaza, ambako alitaja msongamano wa misaada inayolengwa katika eneo la Palestina kuwa ni wa kusikitisha .

Forum

XS
SM
MD
LG