Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:47

Antonio Guterres anatembelea Mpaka wa Misri na Gaza


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Guterres anapanga kurudia wito wake wa kusitisha mapigano kwa ajili ya msaada wa kibinadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kutembelea mpaka wa Misri na Gaza leo Jumamosi, baada ya Israel kuapa kutuma vikosi vyake kupambana na Hamas katika mji wa karibu wa Rafah, hata bila msaada wa Marekani.

Wakati wa ziara yake, Guterres anapanga kurudia wito wake wa kusitisha mapigano kwa ajili ya kibinadamu, ingawa shinikizo la kimataifa hadi sasa limeshindwa kuizuia Israel kutoka kwa mashambulizi ya ardhini yaliyopangwa huko Rafah, ambako idadi kubwa ya watu wa Gaza wamejihifadhi huko.

Licha ya onyo kwamba operesheni kama hiyo itasababisha vifo vya raia wengi na kuzidisha mgogoro wa kibinadamu unaolikumba eneo hilo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema ataendelea na mashambulizi hayo. "Natarajia kufanya hivyo kwa msaada wa Marekani, lakini kama ikibidi, tutafanya hivyo peke yetu", Netanyahu alimwambia waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken siku ya Ijumaa.

Juhudi za kimataifa za kusitisha mapigano ya karibu miezi sita zimeongezeka, huku wizara ya afya katika eneo la Gaza linaloendeshwa na Hamas ikiripoti watu 32,070 waliuawa katika ardhi ya Palestina kufikia Ijumaa na maonyo kadhaa ya Umoja wa Mataifa kuhusu baa la njaa.

Forum

XS
SM
MD
LG