Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:11

Moshi mkubwa watanda Gaza wakati Israel ikiendelea na mashambulizi


Moshi mkubwa watanda Gaza wakati Israel ikiendelea na mashambulizi.)(Photo by SAID KHATIB / AFP)
Moshi mkubwa watanda Gaza wakati Israel ikiendelea na mashambulizi.)(Photo by SAID KHATIB / AFP)

Israel imepania kufanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Hamas huko Rafah hasa kusini mwa gaza, mpango ambao umezusha tahadhari ya kimataifa kwa sababu ya kuwepo uwezekanao wa kuumia maelfu ya raia waliotafuta hifadhi huko.

Israel imepitisha mipango ya kijeshi kwa ajili ya mashambulizi yake.

Lakini wapalestina milioni 1.4 wamekwama katika mji, washirika wa Israel ikiwemo Marekani wametaka uangalizi mkubwa kwa raia katika uvamizi wake unaotarajiwa.

Wizara ya afya ya Gaza imeitaja idadi ya vifo leo inakaribia wapalestina 32,000.

Hospitali kubwa ya Gaza imekuwa kama kitovu kikubwa baada ya Israel kuwashutumu wanamgambo wa palestina kwa kujificha huko na kuanzisha uvamizi wa siku nyingi ambao ilisema Alhamisi umewauwa zaidi ya wapiganaji 140.

Forum

XS
SM
MD
LG