Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, alikuwepo Misri kwa mazungumzo yaliyo jikita katika juhudi za kupatikana kwa sitisho la mapigano kwa vita vya Israel, na Hamas.
Juhudi hizo inajumuisha pia kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa huko Gaza, na kufikishwa kwa misaada zaidi ya kibinadamu ndani ya Gaza kuwasaidia Wapalestina ambao wana shida kubwa.
Wizara ya mambo ya nje imesema waziri Blinken, alijadili uwezekano wa kusimamishwa kwa mapigano kwa walau wiki sita pamoja na kuachiliwa mateka walio salia wakati alipokutana na rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sissi.
Mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani, pia alipanga kukutana na wawakilishi kutoka Jordan, Saudi Arabia, Qatar, na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Nchi kadhaa zimehusika katika mazungumzo ya wiki kadhaa kujaribu kukuballiana juu pendekezo litakalokubalika na wote Israel na kundi la wanamgambo la Hamas.
Forum