Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 09:33

Litakuwa 'kosa' kufanya mashambulizi ya ardhini Rafah, Biden amuambia Netanyahu


Rais wa Marekani Joe Biden (Kushoto) na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.
Rais wa Marekani Joe Biden (Kushoto) na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Rais wa Marekani Joe Biden alimuonya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumatatu kwamba mashambulizi ya ardhini katika mji wa Rafah yatakuwa "kosa," walipozungumza kwa mara ya kwanza ndani ya mwezi mmoja, huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kuhusu vita katika Ukanda wa Gaza.

Katika kile kinachoonekana kama ongezeko la shinikizo la Marekani kwa Israeli, huku idadi ya waliofariki katika ukanda wa Gaza ikizidi kuongezeka na hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbaya, Netanyahu alikubali ombi la Biden la kutuma timu ya maafisa wa ngazi za juu wa usalama wa Israel mjini Washington, kujadili mipango yake ya Rafah.

Lakini Netanyahu alisema amesisitiza kwa Biden kufikia lengo la vita la Israel la kuondoa Hamas -- kundi la wanamgambo wa Palestina waliofanya mashambulizi ya Oktoba 7mwaka jana dhidi ya Israel – kauli yake ikiashiria ugumu wa Marekani kumshawishi mshirika wake mkuu, Israeli.

Viongozi hao wawili walizungumza mara ya mwisho mnamo Februari 15 na Biden ameonyesha kutokuwa na subira na Netanyahu, akihofia kwamba upinzani wa Wamaekani kwa vita vya Gaza unaweza kuharibu nafasi yake ya kuchaguliwa tena mnamo mwezi Novemba.

"Rais alieleza kwa nini ana wasiwasi mkubwa kuhusu matarajio ya Israel kufanya operesheni kubwa za kijeshi huko Rafah," Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa White House Jake Sullivan aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu.

Jumapili Nteanyahu alisema wanajeshi wake wangeendelea na operesheni hiyo licha ya upinzani kutoka kwa jumuiya ya kimataifa akiongeza kwamba "wanamgambo wa Hams ni sharti waangamizwe ili kuondoa tishio katika siku za baadaye."

Forum

XS
SM
MD
LG