Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:09

Netanyahu adai magaidi 13,000 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa katika vita dhidi ya Hamas


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumapili alisema kwamba magaidi wasiopungua 13,000 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa katika vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza na ameapa kuendeleza mashambulizi kusini mwa eneo hilo.

Takriban Wapalestina 31,000 waliuawa huko Gaza katika vita vya Gaza vilivyodumu miezi mitano, ambavyo vilizuka baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel tarehe 7 Oktoba na kuua watu 1,200 na kuwashika mateka 253, kulingana na takwim za Israel.

Wizara ya afya ya Gaza haitofautishi idadi ya vifo kati ya raia na wanamgambo wa Hamas lakini ilisema kwamba asilimia 72 ya wale waliouawa ni wanawake na watoto. Hamas imetupilia mbali takwimu hizo za Israel na kusema ni njama ya kudai “ushindi bandia”.

Netanyahu alikiambia chombo cha habari cha Ujerumani Axel Springer, mmiliki wa magazeti ya Politico na Bild na kituo cha televisheni cha Welt, kwamba kuendeleza mashambulizi ndani ya Rafah kusini mwa Gaza ni muhimu sana kuishinda Hamas.

“Tunakaribia kupata ushindi. Mara tu tukianza operesheni dhidi ya kambi za kijeshi zinazobaki za magaidi huko Rafah, ni suala la wiki hadi awamu ya mapigano makali itakuwa imekamilika,” gazeti la Bild limemnuku Netanyahu akisema.

Forum

XS
SM
MD
LG