Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:57

Jeshi la Israel laripoti kufanya uvamizi na kuharibu makao makuu ya wanamgambo Ukanda wa Gaza

wanajeshi wa Israel wakati wa operesheni ya kijeshi jirani na hospitali ya Al-Shifa Picha na Vikosi vya Ulinzi vya Israeli / AFP
wanajeshi wa Israel wakati wa operesheni ya kijeshi jirani na hospitali ya Al-Shifa Picha na Vikosi vya Ulinzi vya Israeli / AFP

Jeshi la Israel Alhamisi liliripoti kufanya uvamizi na kuharibu makao makuu ya wanamgambo katika sehemu za kusini za Ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israel Alhamisi liliripoti kufanya uvamizi na kuharibu makao makuu ya wanamgambo katika sehemu za kusini za Ukanda wa Gaza.

Jeshi la Ulinzi la Israel limesema wanajeshi wa Israel walifanya operesheni katika eneo la Khan Younis, ikiwa ni pamoja na kutafuta ghala ya utengenezaji silaha.

Operesheni za Israel katikati mwa Gaza pia zilijumuisha mauaji ya wanamgambo 10 katika siku iliyopita, jeshi lilisema.

Kaimu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Palestina alisema Jumatano kwamba Wapalestina wasiokuwa na makazi wamejihifadhi karibu na Rafah, kwenye mpaka wa Gaza na Misri, wameanza kuondoka eneo hilo kwa sababu wanaogopa maonyo ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu uvamizi wa kijeshi ifikapo Ramadhani.

Forum

XS
SM
MD
LG