Akiwa madarakani kama Rais au waziri mkuu tangu mwishoni mwa 1999, Wakala huyo wa zamani wa KGB anashiriki uchaguzi huo kama kuonyesha uaminifu wa raia wa Russia na wanaounga mkono uamuzi wake wa kulishambulia kijeshi taifa la Ukraine, sasa ukiwa ni mwaka wake wa tatu.
Ushindi huo utamruhusu Putin kubaki madarakani hadi 2030, muda mrefu kuliko kiongozi yeyote wa Russia tangu Catherine the Great katika karne ya kumi na nane.
Wakati upigaji kura ulianza, Moscow na Kyiv zilitoa taarifa kuwa raia wameuawa katika wimbi la hivi punde la mashambulizi ya anga ya usiku kucha.
Putin amewataka Wa Russia kumuunga mkono katika hali aliyoitaja kuwa "kipindi kigumu".
Imani ya kiongozi huyo wa Kremlin imeongezeka huku wanajeshi wake hivi karibuni wakiwa wamejipatia ushindi wao wa kwanza wa kieneo nchini Ukraine katika takriban mwaka mmoja.
Serikali za Magharibi na Kyiv wameshutumu zoezi hilo la upigaji kura na kusema ni aibu.
Forum