Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:59

Wizara ya ulinzi ya Russia yasema imeharibu ndege 15 za Ukraine zisizo na rubani na makombora manane

Wakazi wakikusanya vioo vya madirisha vilivyovunjika baada ya mlipuko wa ndege isiyo na rubani ya Russia iliyoanguka katika majengo ya makazi huko Kyiv Novemba 25, 2023, (Picha na Sergei SUPINSKY / AFP)

Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema Alhamisi iliharibu ndege 15 za Ukraine zisizo na rubani na makombora manane, huku maafisa katika eneo la Russia linalopakana na Ukraine wakisema mtu mmoja aliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa na shambulio la ndege isiyo na rubani ya Ukraine.

Vyacheslav Gladkov, gavana wa mkoa wa Belgorod, alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari aliuwawa katika shambulio hilo huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Gladkov alisema ndege nyingine isiyo na rubani iliangukia kwenye mti, huku wimbi la mlipuko likiharibu nyumba mbili lakini hakuna majeruhi.

Huko Ukraine, Oleh Synehubov, gavana wa mkoa wa mashariki wa Kharkiv, aliripoti shambulio la kombora la Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG