Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 20:59

Ukraine yasema Russia imefanya mashambulizi


Ukraine, jumatano imesema duru ya sasa ya mashambulio ya usiku ya Russia, ni pamoja na ndege zisizo na rubani 42, pamoja na makombora matano ambayo yalilenga mikoa minane ya Ukraine.

Kikosi cha anga cha Ukraine kimesema walinzi wa usalama wa anga wa nchi hiyo walitungua ndege 38 kati ya 42.

Mapigano hayo yalifanyika katika mikoa kadhaa ya Ukraine, limesema jeshi la anga la nchi hiyo.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine, amesema watu saba katika mji wa Sumy walijeruhiwa.

Serhiy Lysak, gavana wa mkoa wa Dnipropetrovsk, ameripoti uharibifu wa milingoti ya umeme lakini akasema hakuna aliyejeruhiwa.

Maafisa wa Russia, wamesema kuwa ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine, zilishambulia kituo cha mafuta katika moja ya viwanda kikubwa vya madini ya chuma nchini Russia, leo Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG