Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:02

Russia yamkamata raia wa Korea Kusini kwa madai ya ujasusi


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Raia mmoja wa Korea Kusini alikamatwa nchini Russia kwa madai ya ujasusi, shirika la habari la serikali ya Russia TASS liliripoti Jumatatu.

TASS ilinuku vyombo vya kisheria vikisema, mtu huyo anayejulikana kwa jina la Park Won-soon, alizuiliwa katika mji wa mbali wa mashariki mwa nchi wa Vladivostok kabla ya kuhamishiwa Moscow “kwa hatua za uchunguzi.”

Shirika hilo la habari la serikali limesema ni kesi ya kwanza dhidi ya raia wa Korea Kusini.

Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini ilisema katika taarifa kwamba ubalozi wake mdogo ulimsaidia raia wake tangu ulipopata taarifa ya kukamatwa kwake. Umejizuia kutoa maelezo zaidi kwa sababu suala hilo linaendelea kuchunguzwa.

Russia inaichukulia Korea Kusini kama nchi “isiyo rafiki” kwa sababu ya uungaji mkono wa Seoul kwa vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Moscow juu ya vita vya Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG