Wapalestina wasiopungua 29 waliuawa Alhamisi wakati wakisubiri msaada katika mashambulizi mawili tofauti ya Israel katika Ukanda wa Gaza, wizara ya afya ya Gaza ilisema.
Israel itajaribu kuruhusu msaada wa kibinadamu uingie kwa wingi katika Ukanda wa Gaza kutoka njia mbalimbali, msemaji wa jeshi la Israel alisema Jumatano, huku shinikizo la kimataifa likiongezeka kushughulikia tatizo la ongezeko la njaa katika eneo hilo lililozingirwa.
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan ameliambia jeshi kuwa litaendelea kuteka maeneo zaidi baada ya mafanikio makubwa hivi karibuni katika vita vya miezi 11 dhidi ya kikosi cha Dharura (RSF).
Watu wenye silaha nchini Nigeria waliteka nyara watu 61 katika kijiji kimoja katika jimbo la kaskazini la Kaduna, siku chache baada ya wanafunzi 300 kutoweka katika shambulio la genge lenye silaha, wakazi walisema Jumanne.
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry, amesema atajiuzulu baada ya kuundwa kwa baraza la mpito la uongozi ingawa wakuu wa magenge ya uhalifu wanasisitza juu ya kuhusishwa kwenye mipango yoyote ya kuunda serikali ya mpito.
Polisi wa Sweden Jumanne walimuondoa kwa nguvu Greta Thunberg na wanaharakati wengine wa hali ya hewa ambao walikuwa wanawazuia watu kuingia katika bunge kwa siku ya pili, waliondolewa kwa kuingizwa kwenye gari la polisi.
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry amejiuzulu kama kiongozi wa taifa la Caribbean, kiongozi wa jumuiya ya kikanda na rais wa Guyana alisema Jumatatu usiku.
Raia mmoja wa Korea Kusini alikamatwa nchini Russia kwa madai ya ujasusi, shirika la habari la serikali ya Russia TASS liliripoti Jumatatu.
Mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na muungano wa jeshi la Marekani na Uingereza yalilenga miji ya bandari na miji midogo magharibi mwa Yemen Jumatatu, na kuua watu 11 na kujeruhi wengine 14, msemaji wa serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa ameliambia shirika la habari la Reuters.
Jenerali wa juu wa kijeshi kutoka jeshi la Sudan amefuta uwezekano wa sitisho la mapigano katika mwezi mtukufu wa Ramadan, mpaka pale kundi la kijeshi linalo pigana na serikali litakapo ondoka kwenye maeneo ya raia na umma.
Ukraine Jumapili ilipinga wito wa Papa Francis wa kujadili kusitisha vita na Russia, huku Rais Volodymyr Zelenskiy akisema Papa alikuwa akifanya “upatanishi kwa mbali” na waziri wake wa mambo ya nje akisema Kyiv haitasalimu amri.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumapili alisema kwamba magaidi wasiopungua 13,000 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa katika vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza na ameapa kuendeleza mashambulizi kusini mwa eneo hilo.
Mtoto wa kiume wa mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani nchini Uturuki, ripoti ya chombo cha habari nchini humo imesema.
Ufaransa itabakisha wanajeshi wake nchini Chad, iliyo chini ya utawala wa kijeshi, huku ikiwaondoa kwingineko barani Afrika, kutokana na mvutano na tawala za kijeshi, mjumbe wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Alhamisi.
Tajiri mkubwa sana barani Afrika kutoka Nigeria Aliko Dangote, anapanga kufungua ofisi ya mauzo ya bidhaa za mafuta, ikitarajiwa huenda ikafunguliwa h mjini London, ili kusaidia kuendesha soko la mafuta na bidhaa kutoka kwenye kiwanda chake kipya cha kusafisha mafuta.
Polisi nchini Kenya wamesema Jumanne, kwamba watu wawili wamekufa kwenye ajali kati ya ndege ya chuo cha urubani, na ile ya abiria, kwenye mji mkuu wa Nairobi.
Mswaada dhidi ya ushoga nchini Ghana unaweza kusababisha nchi hiyo kupoteza dola bilioni 3.8 ufadhili kutoka Benki ya Dunia kwa kipindi cha miaka mitano mpaka sita.
Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris Jumapili alitoa wito wa sitisho la mara moja la mapigano katika ukanda wa Gaza na kuishinikiza kwa dhati Israel kuongeza usambazaji wa misaada ili kupunguza kile alichokiita “hali isiyo ya kibinadamu” na “janga la kibinadamu” miongoni mwa Wapalestina.
Zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanachukuliwa kuwa wanene kupita kiasi, hali inayohusishwa na ongezeko la hatari la matatizo mengi ya kiafya, kulingana na makadirio yaliyosahihishwa na kundi la watafiti wa kimataifa wa shirika la afya duniani (WHO).
Marekani Jumatano ilisema "imefadhaishwa mno" na kupitishwa kwa mswada wa sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, na bunge la Ghana, na kuhimiza utathminiwe upya, ili kubaini kama unafuata katiba ya nchi hiyo.
Pandisha zaidi